quinta-feira, 13 de dezembro de 2007

Yeye anayeshuhudia mambo haya anasema, ``Hakika ninakuja upesi!'' Amina. Njoo, Bwana Yesu!

Kisha akaniambia, ``Usiyawekee muhuri maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki maana wakati umekaribia. Mwache atendaye uovu aendelee kutenda uovu, na aliye mchafu aendelee kuwa mchafu; na atendaye mema aendelee kutenda mema na aliye mta katifu aendelee kuwa mtakatifu.''
``Tazama, Ninakuja upesi! Nakuja na tuzo yangu, nimpe tuzo kila mtu kulingana na matendo yake. Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa wisho, Mwanzo na Mwisho.'' Wamebari kiwa wanaoosha mavazi yao ili wapate haki ya kushiriki mti wa uzima na wapate kuingia katika ule mji kupitia kwenye milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye udanganyifu na kuutenda. Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia mambo haya kwa ajili ya makanisa. Mimi ni Shina na Mzao wa ukoo wa Daudi. Mimi ni Nyota ya asubuhi ing'aayo.''
Roho na bibi harusi wanasema, ``Njoo!'' Na kila mtu asi kiaye na aseme, ``Njoo!'' Na mtu ye yote mwenye kiu na aje, na kila anayetaka na apokee zawadi ya maji ya uzima bure. .

Ufunua was Yohana 22

``Kutakuwa na matukio ya ajabu kwenye jua, mwezi na nyota. Hapa ulimwenguni, mataifa yatakuwa katika dhiki na wasi wasi kutokana na ngurumo na dhoruba za kutisha zitakazotokea baharini. Watu watakufa moyo kwa hofu na wasiwasi kuhusu yale wanayoogopa kuwa yataukumba ulimwengu; kwani nguvu za anga zita tikisika. Ndipo wataniona mimi Mwana wa Adamu nikija katika wingu kwa uwezo na utukufu mkuu. Mambo haya yakianza kutokea, simameni imara, mjipe moyo, kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.''

Mbingu na nchi zitatoweka lakini maneno yangu yatadumu daima.'' Siku Ya Mwisho Itakuja Ghafla
Jihadharini msije mkatawaliwa na ulafi, ulevi na wasiwasi wa maisha haya. Kisha siku ikafika pasipo ninyi kutazamia mka naswa! Kwa maana siku hiyo itawakumba watu wote waishio duniani. Kaeni macho na ombeni ili Mungu awawezeshe kuepuka yale yote yatakayotokea na mweze kusimama mbele yangu mimi Mwana wa Adamu.''

Nenhum comentário: